Burundi yazindua kampeni ya pili ya kupima watu virusi kufuatia ongezeko la wagonjwa wa COVID-19
2021-01-12 16:44:00| cri

Serikali ya Burundi jana Jumatatu ilizindua kampeni ya pili ya kupima watu COVID-19 katika nchi nzima kufuatia kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona katika siku za karibuni.

Kampeni hiyo ya siku 30 inafanyika katika mji wa Bujumbura na mikoa mingine kadhaa ambayo imeripotiwa wagonjwa. Waziri wa Afya ya Umma na Mapambano dhidi ya Ukimwi Thaddee Ndikumana amehamasisha watu kushiriki wengi zaidi kwenye kampeni hiyo ili kujua hali zao kwenye shughuli ya ufunguzi.

Ndikumana amesema tangu wiki iliyopita, watu 100 kati ya 5,300 waliokutana na wagonjwa waliothibitishwa kuwa na COVID-19 wamegunduliwa kuwa na virusi hivyo. Aidha amewanasihi watu wa Burundi na wageni wanaoishi nchini humo kuheshimu hatua za usafi wa kunawa mikono kwa sabuni, kuepuka kupeana mikono na kukumbatiana pamoja na kufuata umbali wa kijamii.