Rwanda kesi za udanganyifu mtandaoni zimeongezeka takwimu kutoka Benki Kuu zinaonyesha
2021-01-12 19:19:53| cri

kuongezeka kwa matumizi ya malipo kwa njia ya kidijitali, benki ya simu ya mkononi na benki ya mtandao, kesi za udanganyifu wa mtandao zimeongezeka, takwimu kutoka Benki Kuu zinaonyesha.

Kati ya Januari na Septemba 2020, kesi 141 za udanganyifu wa mtandao ziliripotiwa na Rwf371 milioni iliyohusika. Kati ya hizi, Rwf89m ilipatikana na zaidi ya Rwf280m haikupatikana.

Katika mwaka uliopita katika kipindi hicho hicho, kesi 102 ziliripotiwa na zilihusisha zaidi ya Rwf447m. Kati ya hizi, zaidi ya Rwf166m ilifanikiwa kupatikana.

Hasara inayotokana na udhaifu katika huduma za benki za rununu na malipo pamoja na benki ya mtandao ni kubwa mno.

Benki Kuu ilibaini kuwa hatua kadhaa za kudhibiti udanganyifu zimewekwa ili kuhakikisha udhibiti mzuri wa kila hatua ya mchakato.

Takwimu za Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda zilionyesha kuwa kiwango cha udanganyifu mtandaoni kiliongezeka katika kipndi cha miezi mitatu wakati nchi ilipofungwa kudhibiti maenezi ya Corona, ambayo ilifikia asilimia 72 kiasi cha fedha kulicho ibiwa.