Madaktari wa China waisaida Sierra Leone kuangalia aina mpya ya COVID-19
2021-01-12 18:49:42| CRI

Timu ya madaktari wa China nchini Sierra Leone hivi sasa inafanya kazi na Kituo cha Taifa cha Mwitikio wa Virusi vya Corona (NaCOVERC) kuangalia kama kuna aina mpya ya COVID-19 nchini humo.

Kwa mujibu wa msemaji wa NaCOVERC Solomon Jamiru, timu ya madaktari wa China inatoa msaada mkubwa kuhakikisha maeneo kama ya matibabu, uchunguzi, na mengineyo yanayohusiana na matibabu katika mapambano dhidi ya janga hili. Hata hivyo Bw. Solomon amesema hadi sasa hawajapata mgonjwa yeyote mwenye aina mpya ya COVID-19.

Sierra Leone ambayo maambukizi yake yalionekana kushuka tangu mwishoni mwa Agosti, sasa yamekuwa yakipanda na kurikodiwa karibu kila siku tangu kuanza kwa msimu wa sikukuu ambapo ina jumla ya vifo 77.