Timu ya wahudumu wa afya ya China kusaidia mapambano dhidi ya COVID-19 katika nchi za Niger na Visiwa vya Comoro
2021-01-12 08:58:37| CRI

Timu ya wataalam wa afya kutoka mkoa unaojiendesha wa Guangxi kusini mwa China itaelekea katika nchi za Niger na Comoro baadaye mwezi huu ili kuzisaidia kupambana na virusi vya Corona.

Timu hiyo ya watu 48 inayohusisha wafanyakazi kutoka hospitali katika miji 12 ya mkoa wa Guangxi, itatoa huduma za afya kwa wakazi wa nchi hizo na kusaidia katika hatua za kukabiliana na janga hilo katika miezi 18 itakayokuwa kwenye nchi hizo.

Tangu mwaka 1976, Guangxi imepeleka jumla ya wahudumu wa afya 656 nchini Niger na 139 nchini Comoro.