Rais wa China asisitiza kuhakikisha kujenga kwa pande zote mambo ya kisasa ya kijamaa
2021-01-12 09:15:24| cri

Rais wa China asisitiza kuhakikisha kujenga kwa pande zote mambo ya kisasa ya kijamaa_fororder_1126970918_16104122253991n.JPG

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa, inapaswa kuchukua kwa usahihi fursa ya kipindi kipya cha maendeleo, kutekeleza vizuri dhana mpya ya maendeleo, kuharakisha ujenzi wa muundo mpya wa maendeleo, na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu wakati wa Kipindi cha “Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Miaka Mitano”, ili kuhakikisha ujenzi wa nchi ya kisasa ya kijamaa unapata mwanzo mzuri.

Rais Xi amesema hayo katika Semina maalumu ya makada wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC iliyofanyika katika Shule ya Chama ya Kamati Kuu ya Chama hicho.

Rais Xi amesisitiza kuwa, wananchi ni msingi thabiti na imani imara kwa utawala wa Chama cha Kikomunisti cha China, na ni kwa kushikilia wazo la maendeleo linalotoa kipaumbele kwa wananchi, kushikilia kupata maendeleo kwa ajili ya wananchi, kwa kutegemea wananchi na kuwanufaisha wananchi, ndipo itawezekana kuwa na mtizamo sahihi kuhusu maendeleo na mambo ya kisasa.

Rais wa China asisitiza kuhakikisha kujenga kwa pande zote mambo ya kisasa ya kijamaa_fororder_1126970918_16103786463941n