Wagombea urais wa upinzani nchini Uganda watoa wito wa uchaguzi wa amani
2021-01-13 08:54:51| CRI

Wagombea urais wa upinzani nchini Uganda wametoa wito wa Amani wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika kesho alhamis, Januari 14.

Wagombea hao, Robert Kyagulanyi, Mugisha Muntu na Patrick Amuriat wamesema hayo katika mkutano wa pamoja na wanahabari uliofanyika mjini Kampala, na kuitaka Tume ya Uchaguzi nchini humo kuandaa uchaguzi huru na wa haki. Pia wamewataka wapiga kura kufuatilia miongozo ya kujikinga na virusi vya Corona wanapokwenda kupiga kura, na kuongeza kuwa daima wamewashauri Waganda kuvaa barakoa na kuweka umbali wa kijamii ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

Kyagulanyi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura, huku wakitoa wito wa kuepuka vurugu.