Misri yaondoa zuio dhidi ya safari za ndege za abiria za Qatar
2021-01-13 08:59:59| CRI

Misri imefungua rasmi anga yake kwa ndege za abiria za Qatar kuanzia jana tarehe 12, ikiwa ni alama ya kuondolewa kwa zuio dhidi ya ndege za Qatar lililotekelezwa kwa zaidi ya miaka mitatu.

Mwezi Juni mwaka 2017, Misri, Saudi Arabia, Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu zilitangaza kukata uhusiano na Qatar na kuiwekea vikwazo na zuio kutokana na kuishutumu Qatar “kuunga mkono ugaidi na kuharibu usalama wa kikanda”.