Zanzibar yaadhimisha miaka 57 ya mapinduzi
2021-01-13 09:21:37| cri

 

 

    Sherehe za kuadhimisha miaka 57 ya mapinduzi Tanzania Zanzibar zimefanyika jana jumanne Januari 12.

     Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea mwaka 1964, ambapo utawala wa Sultan wa Zanzibar na serikali yake ya kiarabu uliangushwa.

     Akihutubia taifa kwenye maadhimisho hayo, Rais Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar amewataka wazanzibar wathamini mapinduzi hayo kwa kuzingatia zaidi kile alichokiita mapinduzi ya kiuchumi.

     Ameongeza kuwa Zanzibar ilikuwa na fursa nzuri ya kuongeza nguvu yake ya kiuchumi kwa njia ya kuendeleza uchumi wa buluu na kuimarisha sekta za kilimo, utalii na uvuvi.