Mfanyakazi aliyekataa kufanya kazi za ziada afukuzwa kazini
2021-01-13 12:06:32| cri

Hivi karibuni mfanyakazi mmoja aliyekataa kufanya kazi za ziara baada ya muda wa kazi na kampuni moja ya usambazaji wa vifurushi alifukuzwa kazi, tukio ambalo limefuatiliwa sana na watu.

Habari kutoka mtandao wa Internet zinasema, kijana Xiao Jiang kutoka mji wa Shanghai alijidai kuwa ni mhitimu wa mwaka 2020, alijiunga na Kampuni ya usambazaji wa vifurushi Shentong Express Julai 2 mwaka 2020. Septemba 7 naibu mkurugenzi wa kampuni hiyo alizungumza na Xiao Jiang na kusema kampuni hiyo inawataka wafanyakazi kumaliza kazi zao saa tatu usiku, na kanuni hii inalenga kuwawajibisha wafanyakazi, na kwamba inamtaka Xiao Jiang asitafute mchumba wakati wa umri kama wake. Septemba 9 Xiao Jiang aliambiwa kuwa amefukuzwa kazi kutokana na kukataa kufanya kazi za ziada wakati wa kipindi cha majaribio .

Baada ya hapo Xiao Jiang aliwasilisha ombi kwa Tume ya Usuluhishi ya Mtaa wa Qingpu. Kamisheni ya Usuluhishi ilitoa uamuzi kuwa Kampuni ya Shentong Express ilisimamisha mkataba wa kazi na mfanyakazi wake kinyume cha sheria, na iliamua Kampuni ya Shentong Express kumlipa fidia kwa mujibu wa sheria. Kampuni ya Shentong Express imekata rufaa kutokana na uamuzi huo.