Rwanda: Rwanda yaanza kuuza bidhaa za kilimo UAE
2021-01-13 19:30:17| cri

Rwanda itaanza kuuza bidhaa zake za kilimo katika milki za kiarabu kupitia kwa maduka ya Carrefour.

Chini ya makubaliano ya mwaka jana kati ya Carrefour  na mamlaka ya kuuza nje bidhaa za kilimo ya Rwanda, nchi hiyo itauza ndizi, mananasi na parachichi.

Balozi wa Rwanda katika milki za kiarabu Emmanuel Hategeka  amesema ushirika huo mpya utasaidia wadau kadhaa wakiwemo wakulima na shirika la ndege na Rwanda.

Ushirikiano kati ya NAEB na Carrefour ni nyenzo muhimu kwa wakulima wa Rwand,  wauzaji bidhaa nje na uchumi wa nchi kwa ujumla.    

Aidha mpango huu mpya ni muhimu zaidi ikizingatiwa kuwa Rwanda inalenga kupata dola milioni 130 kutokana na mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo ifikapo mwaka 2024.