Mike Pence amwambia Nancy Pelosi hataomba kutumika marekebisho ya 25 ya kumuondoa rais Donald Trump
2021-01-13 17:09:16| CRI

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence jana alimwandikia barua Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi akisema hataomba kutumika marekebisho ya 25 ya kumuondoa rais Donald Trump, muda mfupi kabla ya baraza la wawakili kulipigia kura azimio la kumtaka afanye hivyo.

Kwenye barua hiyo iliyotolewa jana usiku Mike Pence amesema haamini kwamba hatua kama hiyo ni kwa ajili ya maslahi ya taifa au inaendana na katiba na kumtaka spika Pelosi na kila mjumbe wa Congress kutochukua hatua ambazo zitazidisha mpasuko na kuchochea hali iliyopo sasa. Ameahidi kuendelea kushirikiana kwa nia njema na utawala mpya ujao ili kuhakikisha makabidhiano ya madaraka yanafanyika kwa utaratibu.

Jumatatu Chama cha Democratic kilitoa azimio la kumshtaki Trump kwa “uchochezi wa ghasia”.