Rais wa Indonesia adungwa chanjo ya COVID-19 inayotengenezwa na China
2021-01-13 18:41:14| CRI

Rais wa Indonesia adungwa chanjo ya COVID-19 inayotengenezwa na China_fororder_VCG31N1230557403

Rais Joko Widodo wa Indonesia leo mchana kwenye ikulu yake mjini Jakarta alidungwa chanjo ya COVID-19 inayotengenezwa na kampuni ya Sinovac ya China. Yeye pia ni mtu wa kwanza nchini Indonesia kudungwa chanjo ya COVID-19.

Kituo cha televisheni kilionyesha mchakato kamili wa rais Joko akipigwa chanjo. Baada ya kudungwa sindano ya kwanza ya chanjo hiyo, rais Joko alitoa cheti cha kupigwa chanjo. Baada ya siku 14 atadungwa sindano ya pili ya chanjo hiyo.

Tarehe 7 mwezi huu, rais Joko kwenye tovuti yake ya kijamii alisema anataka kuwa mtu wa kwanza kupigwa chanjo ya kampuni ya Sinovac ya China, ili kuwafanya watu wote waamini chanjo hiyo ni salama.