Thamani ya uuzaji wa bidhaa za kilimo kwenye mtandao wa Internet yafikia karibu bilioni 400 nchini China
2021-01-13 18:42:31| CRI

Baada ya kutekeleza mkakati wa ustawi wa vijiji, mapato ya wakulima wa China yameongezeka kwa miaka mfululizo, na kutimiza lengo la kuongeza mara dufu kuliko mwaka 2010. Biashara ya kidijitali ikiwa mtindo mpya wa uuzaji wa bidhaa za kilimo imehimiza kwa ufanisi ongezeko la mapato ya wakulima.

Naibu waziri wa kilimo wa China Bw. Liu Huanxin kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, kutekeleza mkakati wa ustawi wa vijiji ni uamuzi muhimu wa mkutano wa 19 wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisiti cha China. Miaka mitatu iliyopita, mkakati huo umeanzishwa vizuri, uwezo wa kuhakikisha uzalishaji umeinuka kwa umadhubuti, mapato ya wakulima yameongezeka kwa miaka mfululizo, pengo kati ya mapato ya watu wa mijini na vijijini imepungua.

Mkurugenzi wa idara ya mpango wa maendeleo katika wizara hiyo Bw. Zeng Xiande amesema, mwaka 2019 thamani ya uuzaji wa bidhaa za kilimo kupitia mtandao wa Internet imefikia karibu yuan bilioni 400, ambayo sawa na dola za kimarekani bilioni 61.76, wakulima wengi waliuza bidhaa zao kupitia video mfupi na kuonyeshwa moja kwa moja kwenye mtandao.