UM wataka tahadhari zaidi dhidi ya tishio halisi linaloendelea
2021-01-13 08:53:09| CRI

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Ofisi ya Kupambana na Ugaidi Vladimir Voronkov, jana jumanne ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kudumisha ufuatiliaji dhidi ya tishio halisi linaloendelea sasa.

Akizungumza katika mkutano wa kuadhimisha miaka 20 tangu kupitishwa kwa azimio namba 1373 (2001) la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuanzishwa kwa Kamati ya Kupambana na Ugaidi.

Ameonya kuwa janga la virusi vya Corona limeweka wazi haja ya kuchukua hatua halisi, kwani magaidi wanatumia fursa hiyo kutumia teknolojia mpya na kuungana na makundi ya kihalifu.

Pia amesisitiza haja ya ushirikiano zaidi na mashirika ya kijamii, vijana, sekta ya biashara, na jamii ya wanasayansi, na kuitaka jamii ya kimataifa kuongeza ushirikiano dhidi ya ugaidi.