Malawi yatangaza janga la kitaifa kufuatia ongezeko la kasi la maambukizi ya COVID-19
2021-01-13 09:36:24| CRI

Malawi yatangaza janga la kitaifa kufuatia ongezeko la kasi la maambukizi ya COVID-19_fororder_malawi

Rais Lazarus Chakwera wa Malawi jana alitangaza janga la kitaifa kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Katika hotuba maalum kwa taifa, Rais Chakwera amesema, kufuatia ongezeko kubwa la vifo na maambukizi mapya ya virusi vya Corona, ataitisha mkutano wa dharua kujadili hatua zijazo za kinga na udhibiti.

Pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada kwa Malawi ili kuisaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotokana na janga la COVID-19.