UM wapongeza mkutano kati ya pande pinzani za Libya ili kuimarisha bajeti
2021-01-13 08:59:32| CRI

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL jana Jumanne ilipongeza mkutano uliofanyika kati ya mawaziri wa fedha wa serikali zinazopingana za Libya ili kuimarisha bajeti ya taifa ya mwaka 2021.

Tume hiyo imeueleza mkutano huo kama hatua inayohitajika sana ambayo inahitaji kuendana na juhudi halisi kwenye njia ya kisiasa kuelekea kuunda serikali ya umoja itakayoweza kutekeleza kwa ufanisi bajeti hiyo ya pamoja.