China yapata maendeleo katika kuendeleza injini za roketi kwa ajili ya safari za anga za juu
2021-01-13 08:59:02| CRI

China yapata maendeleo katika kuendeleza injini za roketi kwa ajili ya safari za anga za juu_fororder_0023248155c61986411103

Kampuni ya Sayansi na Teknolojia ya Anga za Juu ya China CASC imetangaza kuwa China inaendeleza injini mpya za roketi kwa ajili ya safari zijazo za anga za juu.Kwa mujibu wa kampuni hiyo inayomilikiwa na serikali ya China, maendeleo yamepatikana kwenye teknolojia muhimu ya injini zenye msukumo mkubwa zinazotumia hidrojeni na oksijeni, ambazo zitatumika kwenye roketi nzito zenye uwezo wa kupeleka tani 140 za mizigo kwenye obiti ya chini ya Dunia.

Roketi hizo nzito za China zitatumika kwenye uchunguzi wa Mwezi, safari za anga za mbali, ujenzi wa miundombinu mikubwa na maendeleo ya raslimali katika anga za juu.