Wapiganaji 7 wa IS wauawa kaskazini mwa Iraq
2021-01-13 09:00:27| CRI

Muungano wa kimataifa wa kupambana na kundi la Islamic State unaoongozwa na Marekani jana Jumanne ulifanya mashambulizi ya anga dhidi ya maficho ya kundi hilo yaliyoko mkoani Kirkuk, kaskazini mwa Iraq, na kuwaua wapiganaji saba wa kundi hilo.

Taarifa iliyotolewa na Kamandi ya Operesheni za Pamoja nchini Iraq, inasema baada ya mashambulizi hayo yaliyofanyika jana alfajiri, vikosi vya usalama vya Iraq viligundua mabomu, vifaa vya mawasiliano na mahandaki kwenye maficho yaliyolengwa.