China yapinga kauli za waziri wa mambo ya nje wa Marekani dhidi ya CPC
2021-01-13 08:53:42| CRI

China imepinga kauli za kashfa zilizotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo dhidi ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na kusema kulaumu na muitenga China hakutaifanya Marekani kuwa taifa kubwa tena.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian jana alipokutana na wanahabari, alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu ujumbe uliotolewa na Pompeo, ambapo alidai kuwa CPC ni tishio kubwa zaidi kwa Umoja wa Mataifa.

Zhao amesema, kuitenga na kuilaumu China hakutaifanya Marekani kuwa taifa kubwa tena, na kwamba vitendo vibaya havitasaidia taswira na hadhi ya Marekani duniani. Ameongeza kuwa, China daima imekuwa mchangiaji wa amani ya dunia, na mtetezi wa utaratibu wa kimataifa, akitolea mfano wa vitendo halisi vya China katika kuunga mkono mfumo wa pande nyingi.