Jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati na waasi warushiana risasi karibu na Bangui
2021-01-13 17:19:22| CRI

Jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati limerushiana risasi na wapiganaji wanaoshukiwa kuwa ni waasi leo asubuhi katika mlango wa kaskazini wa mji mkuu Bangui.

Mapambano hayo yalifanyika katika wilaya ya PK12 ya Begoua, jirani na manispaa ya kaskazini mwa Bangui. Kwa mujibu wa mashuhuda milio mizito ya risasi ilisikika huko Bangui. Pia kulingana na chanzo cha habari ambacho kipo karibu na maeneo ya mapambanao na kuwasiliana na Xinhua, mapigano ya bunduki vilevile yalifanyika huko Bimbo, mlango wa magharibi wa Bangui.

Tangu katikati ya Disemba, makundi yenye silaha yameungana na kufanya mashambulizi dhidi ya serikali. Muungano huo mpya wa waasi, uitwao Muungano wa Wazalendo kwa ajili ya Mabadiliko, umeapa kuingia Bangui.