Tanzania: Watumishi wa Shirika la Viwango watakiwa kuwa waadilifu
2021-01-13 19:30:37| cri

Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe amewataka watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Vipimo (WMA) kufanya kazi kwa uadilifu, weledi  na kuwafikiria wafanya biashara wakati wakitoa huduma kwa wafanyabiashara ili kuendelea kutengeneza taswira nzuri ya bidhaa  za Tanzania katika soko la ndani nan je ya nchi.

Waziri Mwambe aliyasema hayo jjijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na Menejimenti na wafanyakazi wa TBS na WMA alipofanya ziara katika taasisi hizo akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda, Exaud Kigahe pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Waziri Mwambe ameiagiza TBS kufanya ukaguzi wa bidhaa kwa kushirikiana na taasisi nyingine zinazohusika na ukaguzi wa mizigo bandarini na mipakani ili kupunguza muda unatumika kugagua bidhaa hizo,kupunguza mianya ya rushwa na kurahisisha utoaji wa mizigo hiyo kwa haraka.

Aidha, ameitaka TBS kupunguza muda wa kuandaa viwango kutoka miezi 9 hadi miezi 3 na muda wa usajili wa bidhaa na kutoa alama ya ubora kutoka miezi 3 hadi mwezi mmoja ili kuwarahisishia wajasiliamali kuwezakufanya na kukuguza biashara zao kwa urahisi.