Iran yakanusha kauli ya Pompeo kuhusu uhusiano wa Iran na kundi la “Al-Qaeda”
2021-01-13 09:07:30| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif amekanusha kauli iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo, kuwa Iran inahusiana na Kundi la kigaidi la Al-Qaeda.

Amesema kupitia mtandao wa kijamii kuwa, magaidi wote walioshiriki kwenye shambulizi la Septemba 11 dhidi ya Marekani walitoka eneo la Mashariki ya Kati, na hakukuwa na mtu hata mmoja aliyetoka Iran.

Pompeo alitoa kauli hiyo alipohutubia mkutano wa Shirikisho la waandishi wa habari la Marekani huko Washington. Alisema Idara ya upelelezi ya Iran na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) zinaunga mkono shughuli za kundi la Al-Qaeda, na kwamba “Iran ni Makao makuu mapya ya kundi la Al-Qaeda”.