Tanzania: Waliokondisha ranchi na kushindwa kulipa kodi waagizwa kuzirejesha
2021-01-13 19:30:58| cri

Waziri: Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, ameiagiza Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kuwanyang'anya wawekezaji ranchi zote walizokodishwa na kushindwa kulipa madeni.

Ndaki alitoa maagizo hayo katika mkoa wa Mbeya wakati akizungumza na wakulima na wafugaji katika Bonde la Usangu.

Alisema serikali inahitaji ranchi zote zilipe madeni kuanzia Januari 12 hadi Februari 15, mwaka huu na kwamba zitakazoshindwa kulipa, zinyang’anywe na kupewa wawekezaji wengine.

Pia alipiga marufuku kufanyika kwa shughuli za kilimo kwenye maeneo ya ranchi kwa madai kuwa ni kwenda kinyume cha makubaliano ya mkataba.