Miundombinu iliyojengwa na China kuhimiza ukuaji wa uchumi wa Afrika Mashariki mwaka 2021
2021-01-14 09:17:06| cri

Mkuu wa utafiti wa Shirika la Usimamizi wa Mali la ICEA LION, Judd Murigi amesema, miundombinu iliyojengwa na China inatarajiwa kuhimiza ukuaji wa uchumi wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2021.

Bw. Murigi amesema uchumi wa nchi za Afrika Mashariki ulishuka mwaka 2020 kutokana na hatua za kuzuia kuenea kwa janga la virusi vya Corona. Pia amesema sekta za biashara na uchukuzi zinatarajiwa kufaidika na miundombinu iliyojengwa kwa msaada wa China na kuhimiza ufufukaji wa uchumi wa Afrika Mashariki mwaka 2021. Ameongeza kuwa nchi za kanda hiyo zina fursa kubwa kutokana na anuai ya uchumi na pia kutotegemea mauzo ya bidhaa nje ya nchi.