Russia yakanusha shutuma za Pompeo kuhusu uhusiano kati ya Iran na kundi la al-Qaeda
2021-01-14 09:34:03| CRI

Wizara ya mambo ya nje ya Russia imesema, hakuna ushahidi wowote kuwa Iran ina uhusiano na kundi la al-Qaeda.

Mkurugenzi wa idara ya mambo ya Asia ya wizara hiyo Bw. Zamir Kabulov amesema hayo kufuatia waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo kudai kwamba Iran imekuwa kituo kipya cha kundi la al-Qaeda.

Amesema hakuna taarifa zozote zinazothibitisha kuwa Iran ina uhusiano na kundi la al-Qaeda.