Waziri wa afya wa Uturuki apewa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na China
2021-01-14 09:10:38| CRI

Waziri wa afya wa Uturuki apewa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na China_fororder_W020210114358993006999

Waziri wa afya wa Uturuki Fahrettin Koca jana Jumatano alipewa chanjo ya virusi vya Corona iliyotengenezwa na kampuni ya Sinovac ya China. Waliopewa chanjo pamoja naye ni pamoja na wajumbe wa kamati ya sayansi ya kukabiliana na janga la virusi vya Corona nchini humo.

Akiongea kwenye mkutano na wanahabari hapo jana, waziri huyo amesema chanjo ya China ni salama, na wahudumu wa afya nchini Uturuki wataanza kupewa chanjo hiyo kuanzia leo Alhamisi.

Chanjo hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sinovac ya China, ni chanjo ya kwanza ya virusi vya Corona kupewa kibali cha matumizi ya dharura nchini Uturuki.