Biashara kati ya China na Misri yaongezeka kwa utulivu licha ya changamoto za COVID-19
2021-01-14 09:10:12| CRI

Ubalozi wa China nchini Misri umesema kuwa, licha ya changamoto zilizoletwa na janga la virusi vya Corona, thamani ya mauzo ya China kwa Misri ilifikia dola za kimarekani bilioni 12.06 kuanzia Januari hadi Novemba mwaka 2020, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.2 kuliko mwaka juzi kipindi kama hicho.

Thamani ya jumla ya biashara kati ya nchi hizo mbili kwenye kipindi hicho ilifikia dola za kimarekani 12.895, ambayo iliongezeka kwa asilimia 10 kuliko mwaka juzi.