Tanzania iko katika hali ya tahadhari kufuatia ripoti za wimbi jipya la uvamizi wa nzige
2021-01-14 08:58:22| CRI

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Adolf Mkenda, amesema, mamlaka nchini humo ziko kwenye hali ya tahadhari baada ya onyo lililotolewa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kuhusu wimbi jipya la nzige katika nchi jirani ya Kenya.

FAO imesema, wimbi jipya la nzige linalotoka kaskazini mwa Kenya limefika katika Kaunti ya Taita-Taveta, na huenda wakaingia Tanzania baadaye mwezi huu.

Akizungumza kwa njia ya simu na Shirika la Habari la China Xinhua, Waziri Mkenda amesema, wataalam kutoka wizara hiyo na taasisi nyingine husika wamepelekwa kwenye mpaka wa kaskazini wa Tanzania na Kenya ili kukabiliana na uvamizi wa nzige wa jangwani.