Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia auawa kwenye mapambano
2021-01-14 09:08:44| CRI

Jeshi la Ethiopia jana alasiri limetangaza kifo cha aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Seyoum Mesfin kwenye mapambano yaliyotokea jana katika jimbo la Tigray, kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ofisa mwandamizi wa jeshi hilo, Seyoum Mesfin aliuawa pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa bunge la Ethiopia Asmelash Woldeselassie, na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Abay Tsehaye.

Tangu Novemba 4 mwaka jana, Serikali kuu ya Ethiopia imefanya operesheni za kijeshi jimboni Tigray dhidi ya kundi la TPLF lililotawala jimbo hilo, kufuatia kundi hilo kushambulia kamandi ya kaskazini ya jeshi la serikali.