China yatoa barakoa bilioni 224.2 duniani
2021-01-14 16:57:10| cri

China yatoa barakoa bilioni 224.2 duniani_fororder_VCG111313222225

Msemaji wa forodha ya China Bw. Li Kuiwen amesema, kuanzia mwezi Machi mwaka jana mpaka mwishoni mwa mwaka jana, China imetoa bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 67.7 za kukinga janga la COVID-19 kwa nchi za nje.

Miongoni mwao, China imetoa barakoa bilioni 224.2 zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 52.5 ambapo ni sawa na kutoa barakoa 40 kwa kila mtu mmoja duniani.

Licha ya hayo, China pia imetoa mavazi ya kujikinga bilioni 2.31, miwani ya kujikinga milioni 289 na glavu bilioni 2.92. Vifaa hivyo vimewasaidia watu wanaoshughulikia kazi za kupambana na virusi wa nchi mbalimbali kujilinda afya zao.