Benki ya Dunia: maendeleo ya China kuhimizaongezeko la uchumi wa nchi zinazoibuka kiuchumi
2021-01-14 17:18:22| CRI

Ripoti mpya ya Matarajio ya Uchumi wa Dunia iliyotolewa na Benki ya Dunia inaonyesha kuwa, kutokana na kuenea kwa maambukizi ya janga la COVID-19, uchumi wa dunia katika nusu ya kwanza ya mwaka 2021 utaendelea kudidimia. 

Kwenye kongamano kuhusu ripoti hiyo, ofisa mhusika wa benki ya dunia amesema kushuka kwa uwekezaji na kuongezeka kwa madeni ni athari kubwa zinazosababishwa na janga la COVID-19, lakini uchumi wa China umefufuka, huku pia ukihimiza kufufua uchumi wa dunia hasa wa sehemu ya Asia ya Mashariki na nchi zinazoibuka kiuchumi.  Benki ya Dunia inakadiria kuwa thamani ya jumla ya uzalishaji wa China GDP mwaka 2021 itaongezeka kwa asilimia 7.9.