Biashara ya nje ya China yafikia kilele katika mwaka 2020
2021-01-14 17:19:07| CRI

Biashara ya nje ya China yafikia kilele katika mwaka 2020_fororder_VCG111312976882

Takwimu kutoka mamlaka ya forodha ya China zinaonyesha kuwa, thamani ya jumla ya uuzaji wa bidhaa kwa nje na uagizaji bidhaa kutoka nje katika mwaka 2020 imeongezeka kwa asilimia 1.9 kuliko mwaka 2019 na kufikia yuan trilioni 32.16 ambayo ni sawa na dola za kimarekani trilioni 5. 

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, katika mwaka huo, uuzaji bidhaa wa China kwa nje umeongezeka kwa asilimia 4, huku uagizaji bidhaa kutoka nje ukishuka kwa asilimia 0.7.