Afrika yashiriki kikamilifu kwenye uendelezaji wa chanjo ya COVID-19 duniani
2021-01-14 18:48:26| CRI

Bara la Afrika linashiriki kikamilifu kwenye uendelezaji wa chanjo ya COVID-19 duniani pamoja na majaribio ya kikliniki.

Akihojiawa na Shirika la Habari la China Xinhua, Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika Africa CDC Ahmed Ogwel amesema kwa upande wa uendelezaji wa chanjo ya COVID-19, Afrika ina mkakati wake uliozinduliwa mwezi Agosti mwaka jana ukitekelezwa chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika na kituo cha Africa CDC. Ogwell amesema mkakati huo una madhumuni matatu makubwa likiwemo la uendelezaji wa chanjo pamoja na lengo la kuwezesha kupatikana kwa wakati chanjo ya COVID-19 katika bara zima.

Amebainisha dhumuni lingine ni kwamba kuna taasisi katika Afrika ambazo tayari zimeshaanza mchakato wa kuendeleza chanjo ya COVID-19 kwa ajili ya bara la Afrika.