Gary Neville asema sasa Manchester United wanawania ubingwa
2021-01-14 18:27:47| cri

Beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, amesema anashangaa kuona mashabiki wa timu hiyo hawaamini, lakini ukweli ni kwamba sasa wanawania ubingwa.United walikaa kileleni kwa mara ya kwanza juzi baada ya kufanikiwa kuwachapa Burnley bao 1-0 na kufikisha pointi 36, tatu mbele ya Liverpool.

Neville amesema ameona kuwa kundi kubwa la mashabiki wa United hawaamini kama wanaweza kutwaa ubingwa lakini ukweli ni kwamba timu hiyo inaweza kufanya hivyo kwa kuwa sasa ipo kileleni. Huu ni ushindi mkubwa kabla timu hiyo haijavaana na Liverpool Jumapili ijayo kwenye mchezo mwingine mkubwa wa ligi hii.