Rais wa Marekani ashtakiwa “kuchochea uasi”
2021-01-14 09:30:08| CRI

 

    

     Bunge la chini la baraza la Marekani jana limepitisha mswada wa kumshtaki rais wa nchi hiyo Donald Trump kwa “tuhuma za kuchochea uasi”, na kuweka historia ya rais aliyeshtakiwa mara mbili nchini Marekani.

     Mswada huo umepitishwa kwa kura 232 za ndiyo na kura 197 za hapana. Wabunge wote wa Chama cha Democrats na wabunge kumi wa Chama cha Republican akiwemo kiongozi wa tatu wa chama hicho kwenye baraza la chini Bi. Liz Cheney walipiga kura za kuunga mkono kumshtaki rais Trump.

     Kabla ya kupiga kura, spika wa bunge la chini Bi. Nancy Pelosi amesema rais Trump ni “hatari halisi” kwa Marekani.