Watu zaidi ya elfu 20 wakamatwa Afrika Kusini kwa kukiuka kanuni za kukinga COVID-19
2021-01-14 09:09:10| CRI

Waziri wa Polisi nchini Afrika Kusini Bheki Cele amesema jana Jumatano kuwa, zaidi ya watu elfu 20 wamekamatwa nchini humo kutokana na kushindwa kufuata kanuni za zuio tangu Desemba 29 mwaka jana, wakati nchi hiyo ilipoanza kutelekeza ngazi ya tatu ya hatua za kuzuia kuenea kwa janga la virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa waziri huyo, miongoni mwa waliokamatwa, watu 7,500 walishikiliwa kutokana na kutovaa barakoa, huku wengine 834 wakitiwa mbaroni kwa kukiuka zuio la kuuza, kusafirisha au kusambaza pombe.