Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa uchaguzi huru, wa wazi na amani nchini Uganda
2021-01-14 08:57:33| CRI

Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa uchaguzi huru, wa wazi na amani nchini Uganda_fororder_138a8012083816c4808321c355f1f5a0

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa mchakato wa uchaguzi ulio jumuishi, wa amani, na wa wazi nchini Uganda.

Katibu Mkuu huyo ameeleza wasiwasi wake kutokana na ripoti za vurugu na mvutano mkali katika baadhi ya maeneo nchini Uganda, na kuwataka wanasiasa wote na wafuasi wao kujizuia na matumizi ya kauli za chuki, vitisho na mabavu..

Guterres amerejea ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuunga mkono juhudi za nchi hiyo za kuboresha maendeleo endelevu na kujenga siku za baadaye zenye ustawi.

Uchaguzi mkuu wa rais na wabunge unatarajiwa kufanyika hii leo nchini Uganda, huku rais wa sasa wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, aliyekuwa madarakani kwa muda mrefu, akigombea tena kuendelea na wadhifa huo.