Ethiopia yawarejesha nyumbani raia wake 742 kutoka nchi za Mashariki ya Kati
2021-01-14 16:45:55| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia MoFA imesema katika siku za karibuni Waethiopia wapatao 742 wamerejea nyumbani kutoka nchi za Mashariki ya Kati ambapo kutoka Saudi Arabia wamerejea 607 na Oman 135.

Msemaji wa MoFA Dina Mufti amesema wizara inaendeleza juhudi za kuwarejesha nyumbani Waethiopia waliokwama katika nchi mbalimbali za kigeni. Hata hivyo, amesema wizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo matatizo ya kujua mahali walipo katika nchi hizo walizopo na masuala yanayohusiana na vifaa vya COVID-19.

Katika miezi ya karibuni, Ethiopia imeongeza juhudi za kuwarejesha nyumbani raia wake waliopo katika nchi mbalimbali, hii ikiwa ni sehemu ya diplomasia iliyozinduliwa na serikali ya kuzingatia raia.