Uganda leo yafanya uchaguzi wa rais na wabunge
2021-01-14 16:54:49| CRI

Uganda leo yafanya uchaguzi wa rais na wabunge_fororder_VCG111313818864

Uchaguzi wa rais na wabunge nchini Uganda umefanyika leo Alhamis ambapo jumla ya wagombea 11, wakiwemo rais wa sasa Yoweri Museveni wanawania nafasi ya urais kwenye uchaguzi ambao waangaliazi wanauelezea kama ni wa ushindani mkali.

Kura za maoni zimemuweka Museveni na Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, mwanamuziki aliyegeukia siasa, kuwa washindani wakubwa.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo, vituo vya kupigia kura vitafungwa saa 10 alasiri na kufuatia zoezi la kuhesabu kura. Mwenyekiti wa tume hiyo Justice Simon Byabakama amesema matokeo ya uchaguzi yatatangazwa ndani ya saa 48 baada ya kumaliza zoezi la kupiga kura.