China kubadilisha hekta milioni 6.7 za ardhi yenye chumvi na alkali kuwa mashamba ya mpunga
2021-01-15 18:58:41| CRI

China kubadilisha hekta milioni 6.7 za ardhi yenye chumvi na alkali kuwa mashamba ya mpunga_fororder_VCG111302610850

Timu ya mtaalamu maarufu wa kilimo wa China Yuan Longping leo imetangaza kuwa, inapanga kulima mpunga unaoweza kuvumilia chumvi na alkali katika hekta milioni 6.7 za ardhi yenye chumvi na alkali nchini China katika miaka 8 hadi 10 ijayo.

Timu hiyo imesema imesaini mkataba wa kuendeleza ardhi ya hekta laki 4 yenye chumvi na alkali nchini China.

Timu ya Bw. Yuan imefanikiwa kuchunguza mpunga unaoweza kuvumilia chumvi na alkali mwaka 2017, na kupata rekodi ya juu zaidi ya mavuno ya tani 12 kwa kila hekta mjini Jiangsu mwaka jana.

China kubadilisha hekta milioni 6.7 za ardhi yenye chumvi na alkali kuwa mashamba ya mpunga_fororder_VCG111302610848