Rais wa Uturuki apata chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na China
2021-01-15 09:27:16| cri

Rais wa Uturuki apata chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na China_fororder_202101142326335475

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki jana usiku huko Ankara amepata chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na Kampuni ya SINOVAC ya China.

Rais Erdogan amesema, wajumbe wa kamati ya utendaji ya chama tawala cha AKP nchini Uturuki walipata chanjo hiyo pamoja naye, na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa na wabunge kuwahimiza raia kukubali na kupata chanjo ya COVID-19.

Jumatano wiki hii, Waziri wa afya wa Uturuki alipata chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na Kampuni ya SINOVAC, na mchakato huo pia ulitangazwa moja kwa moja kwa njia ya televisheni.