WHO: Jopo la wataalamu wa kimataifa lafika Wuhan, huku wawili wakishindwa kwenda baada ya kuwa na matokeo chanya ya IgM
2021-01-15 18:51:54| CRI

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus jana alisema, wataalamu 13 wa kimataifa wa kutafuta chimbuko la virusi vya Corona wamefika Wuhan, China wakitokea Singapore, na watashirikiana na wenzao wa China kufanya utafiti wa kujua chimbuko la virusi hivyo. Wataalamu wengine wawili walishindwa kwenda Wuhan baada ya kuwa na matokeo chanya ya vipimo vya IgM.

Bw. Tedros amesema, wataalamu hao walifanya vipimo mara nyingi kabla ya kufunga safari, na matokeo yote ni hasi. Wataalamu waliofika Wuhan kwanza watakaa karantini kwa wiki mbili, ambapo watafanya kazi na wenzao wa China kupitia mtandao. Baada ya karantini, watafanya kazi huko Wuhan kwa wiki mbili.