Maonyesho biashara yaongezwa muda
2021-01-15 19:24:19| cri

Zanzibar imesema imeitikina ombi la wafanyabiashara la kuongezewa siku mbili zaidi ya maonyesho ya Saba ya Biashara Zanzibar.

Akizungumza na uongozi wa Wizara ya Biashara pamoja na Kaimu Waziri wa Wizara ya Biashara , rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi Mudrik Soraga, amesema maonyesho hayo yataendelea kwa siku mbili kwa siku zingine mbili.

Baada ya kutembelea maonyesho, rais Mwinyi alisema amevutiwa na bidhaa mbalimbali zinazouzwa na wafanyabiashara kadhaa wakiwamo wajasiriamali wa ndani na nje na kusisitiza haja ya wizara kuendelea kuwaunga mkono.

Aidha Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwasikiliza wajasiriamali aliowatembelea kwa niaba ya wenzao kuzungumzia mafanikio waliyoyapata katika shughuli zao pamoja na changamoto walizo nazo.

Mwinyi aliwaahidi wafanyabiashara hao wakiwamo wajasiriamali hao kwamba changamoto zinazowakabili zitafanyiwa kazi kwa lengo la kupata mafanikio zaidi.