UM wasema Wairaq milioni tatu wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa usalama wa chakula
2021-01-15 09:12:48| cri

Gazeti la Serikali ya Iraq al-Sabah limeripoti kuwa, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa, karibu Wairaq milioni tatu, wakiwemo wakimbizi wa ndani 731,000 na wale waliorejea, wanakabiliwa na ukosefu wa chakula kutokana na athari za COVID-19, na kushuka kwa bei ya mafuta mwaka 2020. 

Mwakilishi wa WFP nchini Iraq Abdirahman Meygag amesema, uchumi wa Iraq bado unategemea mafuta, na kwamba kushuka kwa bei ya mafuta duniani na hatua ya OPEC kushusha uzalishaji kumekuwa na athari ya moja kwa moja kwa raslimali za chakula. Pia amesema, kushuka kwa thamani ya sarafu ya Iraq kumeathiri bei ya bidhaa za msingi za chakula, hivyo serikali ya Iraq inahitaji msaada kushughulikia tatizo hilo, ikiwemo kutoa ruzuku ya chakula cha msingi na kudhibiti bei.