Russia yaishutumu Marekani kuzuia fursa za mazungumzo kati ya Iran na nchi za Ghuba
2021-01-15 09:02:20| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov amesema jana kuwa Marekani inafanya kadri iwezavyo kukwamisha fursa yoyote ya mazungumzo kati ya Iran na nchi za Ghuba ya Uajemi. Amesema, serikali ya sasa ya Marekani imefanya kila kinachowezekana kuzuia kufanyika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambayo yanaendana na maslahi ya kikanda na kimataifa.