Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Xi Jinping leo amekagua maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki kwa Walemavu mjini Beijing.
Rais Xi Jinping alitembelea Uwanja wa ndani wa Michezo la Mji Mkuu Capital Indoor Training Stadium ulioko kwenye eneo la Haidian, Beijing, na Kituo cha Kuteleza juu ya Theluji alpine skiing cha Taifa na Kituo cha Snowmobile na Sled cha Taifa, ili kupata ufahamu kuhusu hali ya ujenzi wa majumba na viwanja vya michezo na maandalizi ya wanamichezo, kuwatembelea wanamichezo na makocha na timu za utoaji wa huduma za viwanja vya michezo huko Yanqing, pamoja na wawakilishi wa wajenzi.