Mwanaume mmoja alifukuzwa kazi kwa kutohudhuria sherehe ya Siku ya Kuzaliwa ya mfanyakazi mwenzake
2021-01-19 21:04:22| cri

Wakati wa Janga la Virusi vya Corona, wakazi wa sehemu nyingi wanaagizwa kupunguza fursa za kwenda nje, kwa sababu mkusanyiko husaidia kuenea kwa virusi. Hivi karibuni tukio moja la mtu aliyeamua kukaa nyumbani limefuatiliwa sana na watu, baada ya kuathiri kazi yake.

Januari 16 mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 22 huko Guiyang, mkoani Guizhou, ambaye alijiunga na kampuni moja ya uuzaji wa nyumba alifukuzwa kazi kutokana na kutohudhuria sherehe ya Siku ya Kuzaliwa ya mfanyakazi mwenzake. Wanaume wengine wanne walitozwa faini ya yuan 100 kila mmoja, sawa na dola za kimarekani 15 kwa kutohudhuria sherehe hiyo. Tukio ambalo limezusha mjadala makali kati ya wanamtandao.

Ni jambo linalowasumbua wafanyakazi wengi wa kawaida wa ofisi kwa kuhudhuria au la sherehe za siku ya kuzaliwa ya wafanyakazi wenzao, na kutoa au la pesa kwa ajili ya sherehe kama hizo. Mwanaume huyo alikataa kwenda kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa mfanyakazi mwanzake kutokana na wasiwasi wa kuambukizwa virusi, na mfanyakazi mwenzake alimwelewa. Lakini bila kutarajiwa, usiku huo meneja mkuu wa kampuni alitangaza kwenye mtandao wa kijamii wa Wechat kuwa “Kila mtu ambaye hakuhudhuria sherehe hiyo anapaswa kupigwa faini ya yuan 100”.

Siku iliyofuata Xiao Cui hakusema lolote kwa siku nzima, lakini katika mkutano baada ya kazi, meneja huyo alimlenga Xiao Cui na kumwuliza kwa makusudi kama anakubali kutoa faini au la? Xiao Cui alisema hakukubali. Meneja huyo alisema kama hakubali basi atatozwa faini nyingine ya adhabu ya ya yuan 200. Xiao Cui alikataa pia kwa sababu alikuwa amepata ruhusa ya mfanyakazi mwenzake mwenye siku ya kuzaliwa. Meneja alikasierishwa na Xiao Cui na kusema kumtoza faini ya yuan 400, na baada ya hapo alitangaza kuwa Xiao Cui amefukuzwa kazi.