Ni kweli Twitter imemfungia Trump kwa kukiuka maadili na wajibu wa uhuru wa habari?
2021-01-19 18:14:36| cri

  Uamuzi uliochukuliwa hivi karibuni na kampuni ya Twitter kumfungia kabisa Bwana Donald Trump umezua mjadala kuhusu hali, wajibu na hata mamlaka waliyonayo wamiliki wa mitandao ya kijamii. Pamoja na kuwa nchi za magharibi (hasa Marekani) zimekuwa zikijidai kuwa ni vinara wa uhuru wa vyombo vya habari, kitendo cha kumwacha Bw. Trump aendelee kutumia akaunti yake vibaya kwa miaka minne huku akipuuza wajibu wake, kinaonesha kuwa baadhi ya watu wanaweza kuvunja kanuni na kupuuza wajibu wao bila kuchukuliwa hatua, lakini pia kitendo cha kampuni ya Twitter kumfungia Bw. Trump wakati anamaliza muda wake madarakani bila hata kumpa nafasi ya kujitetea, mbali na kuonyesha madaraka makubwa kupita kiasi waliyonayo wamiliki wa mitandao ya kijamii, pia kinaonesha kuwa maslahi ya kiuchumi na sio maadili na wajibu ndio vinaongoza vyombo hivyo.