Tanzania yataka wafugaji kutumia mifugo chotara
2021-01-22 18:28:44| cri

Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) imewataka wafugaji nchini humo kutumia teknolojia ya ufugaji wa kuchanganya mifugo ya asili na chotara ili kubadilisha aina ya mifugo.

Mtafiti Msimamizi wa Idara ya Ng'ombe wa kituo cha Mpwapwa Deogratius Masao amesema teknolojia ya uzalishaji madume na kupandikiza kwa ng'ombe wa asili itasaidia wafugaji wengi kupata mifugo bora ambayo itakakuwa ikitoa maziwa mengi na nyama.

Alisema wao kama kituo cha utafiti, wamekuwa wakielimisha jamii ya wafugaji kuhakikisha wanatumia teknolojia hiyo ambayo itawasaidia kubadilisha ufugaji wanaofanya kadri siku zinavyokwenda.