UNHCR yasema zaidi ya wakimbizi 357,000 kutoka Sudan Kusini wamerudi nyumbani katika miaka mitatu iliyopita
2021-01-22 09:03:13| CRI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema wakimbizi 357,450 kutoka Sudan Kusini wamerudi nyumbani kutoka nchi za kikanda walizokimbilia tangu mwezi Novemba mwaka 2017.

Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 61 ya wakimbizi hao wamerudi kwa hiari kutoka Sudan, huku asilimia 23 wakirudi kutoka Ethiopia.